Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 10, 2010

BANA MWAMBE KUREKODI ALBAM MPYA YA ZINGZONGI


Kiongozi wa bendi ya Bana mwambe shukulu majaliwa


BENDI ya muziki wa Dansi, Bana mwamba 'Zing Zongo' inatarajia kuingia Studio kukamirisha albamu yao mpya ya 'Mke wangu anacheka' itakayokuwa na jumla ya nyimbo sita.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kiongozi wa bendi hiyo Shukuru Majaliwa alisema bendi hiyo ambayo inatamba na mtindo wake wa Bana Mwambe itakamirisha albamu hiyo mwanzoni mwa mwezi ujao.

Alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo kama Yatima hadeki, Kila siku matatizo, Daudi Mchimba kisima, Mwafatima, Furaha ya dewa, na Yatima Hadeki utakaobeba jina la albamu.

"Tunatarajia kuingia Studio kuanza mara moja kurekodi nyimbo hizi ambazo zitaunda albamu yetu mpya na tayari hadi sasa tumeandaa midundo na tumeingia mkataba na FK Meters ya kariakoo kuanza kusambaza albamu yetu mara itakapokamilika.," alisema.

Alisema bendi hiyo ambayo iliwahi kutumikiwa na TX Moshi William ambaye kwa sasa ni marehemu itarekodi albamu yake hiyo katika Studio za Gheto Sound Production zilizopo Masaki Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...