Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 27, 2010

Muthungu atwaa blackberry ya Zain
Mwandishi wetu

David Muthungu ameibuka bingwa wa mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya gofu vya Lugalo vya jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 38 na kumzidi mchezaji mkongwe wa mchezo huo Gidion Sayore kwa tofauti ya pointi 3 Sayore alipata pointi 35.

Mashindano hayo yalikuwa na msisimko mkubwa kutokana na wachezaji wengi walioshiliki kucheza kwa makini, ongezeko la wachezaji kila wiki liliwapelekea wadhamini wa mashindano hayo kampuni ya simu za mkononi ya Zain kuboresha zawadi za michuano hiyo.

Muthungu aliyekuwa akipambana vikali na wachezaji wenzie aliibuka mshindi kwa kishindo na kujinyakulia simu ya mkononi ya blackberry kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Zain.

“Kwanza na mshukulu mungu kuniwezesha kushinda simu kwani siku nyingi nimekuwa nikiwaza lini nitashinda na mimi simu, nimezoea kushinda zawadi za kawaida lakini leo mawazo yangu yamekamilika, pia nawapongeza Zain kwakujaribu kuboresha zawadi za mchezo huu pia na kuufanya mchezo huu upendwe na watu wa rika zote,” Alisema Muthungu.

Mbali na Muthungu washindi wengine walikuwa ni Peter Muchiri,Alex Kobia, Stephani Sayore wote walijipatia zawadi mbalimbali kutoka Zain vikiwemo vyombo vya nyumbani, begi za kisasa miamvuli.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...