Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 23, 2010

KALUNDE KUITEKA MAPUTO


BENDI ya muziki wa dansi ya Kalunde imepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza Jijini Maputo nchini Msumbiji.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana Rais wa bendi hiyo Deo Mwanambilimbi alisema itatumbuiza Oktoba 2 mwaka huu.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa bendi hiyo inatarajia kuondoka nchini Oktoba Mosi na wanamuziki wake wote.

“Tumepata mwaliko wa kwenda kutumbuiza kwenye moja ya tamasha ambalo hufanyika kila mwaka hivyo tunatarajia kwenda kupiga nyimbo zote za Kalunde” alisema Mwanambilimbi.

Alisema mwaliko huo umekuja baada ya baadhi ya mashabiki wa bendi hiyo kuvutiwa na nyimbo wanazopiga.

Kalunde kwa sasa inatamba na nyimbo za ‘Itumbangwewe’, ‘Hilda’, ‘Nataka Kuzaa na Wewe’ , ‘Usiniguse’ ,’Fikiria’ na ‘Kilio Kilio’.

Pia imetoa vibao viwili vipya ambavyo ni ‘Fungua’ na ‘Maiwane’ ambazo tayari zimeanza kutamba katika kumbi za burudani ambazo bendi hiyo inapopiga.

Baadhi ya wanamuziki watakaoondoka na bendi hiyo ni Mwanambilimbi mwenyewe, Shehe Mwakichui, Junior Gringo, Deborah Nyangi, Sarafina Mshindo, Mwapwani Yahya, Othman Majuto na Remmy.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...