Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 19, 2010

CHADEMA WATIKISA JIJI LA ARUSHA


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maelendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia moja ya mikutano minne ya hadhara ya kampeni jijini Arusha jana. (Picha na Joseph Senga)

Mmoja wa wakzi wa jiji la Arusha, akiupungia mikono msafara wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, uliokuwa ukipita katika mitaa ya jiji hlo akiwa katika kampeni zake jana. (Picha na Joseph Senga)
Sehemu ya maelfu ya wakzi wa mji wa Arusha, wakimpungia mikono mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika jana.Mgombea ubunge wa jimbo la Monduli, Mchungaji Molleli Silanga Aman, akisoma biblia wakati wa mkutano wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mjini Arusha jana, mara baada ya kutambulishwa, ambaye alidai kufanyiwa vitisho na mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Edward Lowassa

Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei, akiwahutubia wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake, katika moja ya mkutano wahadhara wa kampeni za mgombea wa urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, jana. (Picha na Joseph Senga)


Wanachma na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakisindikiza gari lililombeba mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mara baada ya mkutano wake wa kampeni jijini Arusha jana. (Picha na Joseph Senga)

Baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha wakimsikiliza mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, wakati wa mkutano wa kampeni zake jijini humo jana. (Picha na Joseph Senga)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...