Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 7, 2010

MSONDO KUTUMBUIZA IDDI MOSI TTC CHANG'OMBE IDDI PILI ZANZIBAR


kundi zima la msondo ngoma likiwa katika picha ya pamoja

Rapa wa msondo ngoma Romani Mng'ande akirapu na kucheza sambamba na nacho Mpendu Mama Nzawisa

muhidini ngurumo akizungumza na waandisha wa habari wakati wa kukabidhiwa vyombo vipya na kampuni ya bia Tanzania kulia ni Meneja wa bia ya SAfari Fimbo Butallah

BENDI ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music Band, inatarajia kufanya onyesho la aina katika Ukumbi wa TCC Chang'ombe, iyotarajia kufanyika siku ya Iddy ambayo itakuwa mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza na gazeti hili, Msemaji wa Msondo Ngoma, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa onyesho hilo linatarajia kuwa la aina yake.

Amesema kuwa onyesho hilo linatarajiwa kuanza mapema ili kuweza kutoa burudani safi kwa wadau na wapenzi wa muziki huo.

Amesema kuwa katika onesho hilo pia kuwa Msondo Ngoma itaimba nyimbo mbili mpya ambazo hazijawahi kusikika mahali popote.

Amesema kuwa nyimbo hizo ambazo wamezitunga wakiwa kambini Amana Ilala wakati walipokuwa katika mfungo wa Ramadhan.

Amesema kuwa pia bendi hiyo itaimba nyimbo mbalimbali za zamani pamoja na zile mpya ambazo zitakuwepo katika albam yao inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

"Tunatarajia kufanya onesho la aina yake wakati wa siku kuu ya Iddy kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki wetu baada ya kupumzika kwa mwezi mzima wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan" alisema Super D.

Amesema kuwa siku ya Iddy Pili wanatarajia kufanya onyesho jingine la aina yake katika Ukumbi wa Gymkhana Klabu uliopo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...