Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 27, 2010

Superbrands yaingia rasmi TanzaniaMkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi, Meneja wa Tanzania Distilleries Limited KONYAGI Bw. David Mgwassa

Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Ajay Mehta.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mtahaba.

Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinazotambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi. Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kampuni ya Azam Bw. Yusuph Kamau katikati ni Meneja Biashara wa kampuni hiyo ya Azam Bw. Daniel Hill aliyembatana nae.


Dar ES Salaam Taasisi ya Superbrands, ambayo ni taasisi kubwa kuliko zote duniani inayoratibu ubora na thamani ya nembo za bidhaa, hatimaye imeingia rasmi nchini Tanzania, bwana Jawad Jaffer, Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands ametamka hivi majuzi. Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na taasisi hiyo, Superbrands inathaminisha nembo ambazo zinatambulika kuwa zenye viwango vya ubora wa juu zaidi kupitia mipango yake mbali mbali. Taasisi hii pia inachapisha vitabu na majarida yanayoelezea shughuli za uimarishwaji na uthaminishwaji wa nembo mbali mbali duniani kote. Superbrands ilizindua miradi yake kwenye masoko makuu mengi duniani kote na inatoa machapisho mbali mbali kwenye takriban nchi 82. Taasisi hii iliingia rasmi Afrika Mashariki mwaka 2007.

Bwana Jawad amesema kwamba taasisi yake itafungua rasmi milango yake kwa makampuni ya Tanzania siku ya Jumatatu, Septemba 27, 2010, siku ambayo itakuwa na matukio mbali mbali muhimu, kama vile hotuba zitakazotolewa na wawakilishi wa Superbrands na Maofisa Watendaji Wakuu wa kampuni za Kitanzania. Hafla hiyo itaambatana pia na hafla ya utoaji wa tuzo za ubora za Superbrands kwa baadhi ya kampuni za Kitanzania ambazo tayari zimethaminishwa kuwa na kiwango cha juu cha ubora wa huduma na bidhaa zao.

Akiongea na waandishi wa habari, bwana Jawad amesema kwamba alikuwa mmojawapo wa watendaji wakuu wa kamati iliyoundwa kuendeleza Nembo ya Kenya, amesema kwamba kwa sasa anaweka mkazo zaidi katika utashi wake wa kuendeleza nembo za kampuni zilizopo Afrika Mashariki ili kuziwezesha kutambulika duniani kote. Amesema kwamba ameichagua Tanzania kuwa kambi kuu ya mkakati wake huo.

Akizungumzia jinsi Superbrands inavyofanya kazi yake, Jawad ameeleza kwamba jambo la kwanza linalofanyika ni kuandaliwa kwa orodha ya nembo za kampuni zinazoongoza na kufanya mchujo hadi kupatikana zile zilizo bora zaidi. Akaongeza kwamba, kinachofuata, baraza maalum la wataalam kutoka kwenye sekta za habari, masoko, utangazaji na mahusiano ya umma, hukutana na kuzipigia kura kila nembo itakayotauliwa, na kuziweka kwenye kiwango cha alama kuanzia namba 1 hadi 10. “Baraza huangalia vipengele vingi kama vile uaminifu wa wateja, kukubalika kwa jumla kwa nembo kwenye soko, muda wake kwenye soko na uimara wake,” Jawad alisema. Alisema, nembo zitakazopata alama za juu kabisa ndizo zinazochaguliwa na kuteuliwa kupata Hati ya Ubora ya Superbrands. Baada ya hapo, walaji (watumiaji) wanaombwa kuzipigia kura nembo hizo kwa vigezo vya umahiri wa nembo, ubora na uzatiti wake.

“Tunapopata maoni ya walaji na ya baraza la wataalam, tunapata mitazamo miwili tofauti ambayo tunaijumuisha ili kupata mtazamo wa jumla wa nembo husika,” alisema bwana Jawad. “Kwa mwendendo huu, tunaweza kupata nembo zenye ubora wa ziada kutoka kwenye kundi la nembo zenye ubora wa kawaiday,” aliongeza.

Kwenye utafiti uliofanyika kwenye kipindi cha mwaka 2007-2008, jumla ya watu 900 walihojiwa nchini Kenya, watu 700 walihojiwa nchini Uganda, na watu 900 walihojiwa nchini Tanzania. Utafiti huu ulifanyika kwenye miji mikuu ya nchi hizi, na ulijumuisha nembo 64 zilizo maarufu zaidi Afrika Mashariki, zilizoonekana kwenye toleo la kwanza la jarida la Superbrands, linalotambua nembo mahiri zaidi kwenye ukanda huu. Kitabu hicho kinajumuisha maelezo juu ya nembo mahiri tofauti, kama vile historia, masoko, mafanikio, bidhaa, matukio mapya, uhamasishaji na thamani ya nembo. Kwa mujibu wa utafiti huo, nchini Tanzania, nembo zilizopata nafasi kumi za juu zilikuwa Azam (1), Nokia (2), Blue Band (3), Tigo (4), VodaCom TZ (5), Kilimanjaro Pure Drinking Water (6), Whitedent (7), University of Dar es Salaam (8), Chai Bora – TATEPA (9), na Omo (10).

Japokuwa utafiti huo unaofanyika Afrika Mashariki sio wa muda mrefu sana, Superbrands inaendesha mkakati wake huu kwa mara ya pili hapa Afrika Mashariki, ikitarajia kwamba toleo la pili la jarida la Superbrands kuchapishwa mwaka huu wa 2010.

Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Jawad alisema kwamba changamoto kubwa analokutana nalo wakati wa utendaji wake wa kazi ni uelewa mdogo wa masuala ya nembo za kibiashara miongoni mwa wadau mbali mbali. Ili kukabiliana na changamoto hii, amesema kwamba Superbrands Afrika Mashariki ina mpango wa kuendesha kampeni ya uhamasishaji kwenye uwanda huu, ambapo vitabu vitasambazwa kwenye makampuni na taasisi mbali mbali, hususan vyuo vinavyotoa mafunzo ya kibiashara ili kuongeza uelewa na ufahamu na maarifa kuhusu masuala ya nembo na uendelezaji wa nembo. Amesema mkakati huu utawavutia, hususan, wamiliki wa viwanda ambao tayari wameziona jitihada hizi kama mojawapo ya njia ya kuzitambulisha shughuli zao kwa wanafunzi na hivyo kuimarisha uingizwaji wao kwenye mfumo wa utendaji kazi, ikilinganishwa na mikakati mbali mbali ya mafunzo yanayoendeshwa kwa ajili hiyo kila mwaka. Jawad amesema kwamba tayari kuna mifano hai ya utafiti juu ya nembo zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ambayo inatumika kama sehemu mojawapo ya mafunzo kwenye vitivo vya biashara kwenye vyo vikuu nchini Kenya.

Akiendelea na maongezi, Jawad amesema kwamba hivi sasa kuna mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa kwenye uendezwaji wa harakati za uimarishaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jambo ambalo linahitaji kampuni kujenga uelewa na ufahamu wa nembo zao nje ya mipaka ya nchi zao. Alisema kwamba baada ya miaka miwili suala la nembo litakuwa ni jambo muhimu sana.

“Tunachotaka kufanya ni kuziendeleza nembo zaidi ya kile unachokiona kila siku. Tunaitaka serikali kusaidia kusogeza mbele nembo zinazoheshimika ili kuwasaidia watu kuzielewa,” alisema. Jawad alisema pia kwamba anataka nembo za Afika Mashariki kutambulika katika ngazi ya kimataifa. “Kwa kuhamasisha utambuzi na uelewa wa nembo tutakuwa tumechangia jambo hilo kufanikiwa,” alisema. Alisema anasikitika kwamba nembo za Afrika Mashariki hazijafikia hatua ya kuweka alama ya kijiografia, wakati kuna nembo ambazo ni vichocheo muhimu vya uchumi wa nchi zilizoendelea.

Akielezea juu ya faida ambazo Superbrands inazipatia kampuni, Jawad amesema kwamba Superbrands inachangia kwa kiwango kikubwa kuwapo kwa utambuzi na uelewa wa nembo, ambapo kupitia machapisho yake, maelezo juu ya kampuni za Afrika Mashariki yanasambazwa ndani ya Afrika Mashariki na nje yake. Maelezo yanayopatikana kwenye machapisho ya Superbrands zinaweza kuwa chanzo cha taarifa kwa watu binafsi au taasisi ambazo zinataka kuwekeza kwenye kampuni, alisema.

Bwana Jawad alisisitiza kwamba Superbrands pia ni kichocheo cha mauzo, kwani kampuni zinaweza kutumia maelezo yanayochapishwa juu yake kuimarisha mahala pake na kujijengea mkakati wa upanuzi wa soko lake. Alionesha mfano wa utafiti uliofanyika muda si mrefu uliopita nchini Uingereza, ambao ulibainisha kwamba wateja wanakuwa wepesi zaidi kununua bidhaa au huduma yenye nembo rasmi ya Superbrands, kuliko zile ambazo hazina chapa hiyo. Mtazamo kwamba baadhi ya nembo za Kenya zinatambulika sana nchini Uganda na Tanzania unaweza kuisaidia nembo kufikiriwa kupenyeza kwenye masoko ambayo mafanikio mazuri yanatarajiwa.

Akihitimisha, bwana Jawad alisema kwamba Superbrands inachangia utoaji wa maamuzi wa watendaji wakuu wa makampuni, akibainisha kwamba Superbrands inaipa nembo hadhi kubwa ambayo ni ujumbe wenye nguvu kubwa kwa wateja wa kibiashara, waajiriwa na wanahisa.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na bwana Jawad wa Superbrands Afrika Mashariki ___________________________________.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...