Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 6, 2010

Mwandishi Dar Leo aula Sifa Politan


Na Mohamed Akida,Temeke


MWANDISHI wa habari wa gazeti la Dar Leo linalochapishwa na Kampuni ya Business Times Limited (BTL), Victor Mkumbo, amechakuwa kuwa msemaji wa timu ya Sifa Politan ya Temeke katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Temeke, jana.

Katika uchaguzi huo, Mkumbo alijizolea kura 34 za wajumbe wote waliopiga kura katika mkutano huo baada ya kukosa mpinzani katika nafasi hiyo.

Katika uchaguzi huo, nafasi ya Mwenyekiti ilichukuliwa na Mohamed Mwinyi ambaye alipita bila kupingwa huku Hija Hamidu akishinda nafasi ya Mwenyekiti msaidizi.


Ally Mshindo alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu na Mwinyimvua Said akiwa msaidizi wake, Mhazini alichaguliwa Awadhi Mukhisin ambaye atasaidiwa na Makame Salehe.

Mwakilishi wa soka la Wanawake na Vijana ni Selemani Mkati, na wajumbe ni Cycacus Rweyemamu, Riziki Hamis, Habibu Mbunga, Samson Boniventure, Ally Kilindo, Zuber Mbeba na Salumu Mbugalo.

Mara baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Mohamed Mayosa, aliwashukuru wajumbe hao kwa kuchagua viongozi wao watakaowaongoza kwa mujibu wa katiba ya klabu hiyo. stori na picha kwa hisani ya dar leo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...