Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 14, 2010

BASATA YAWAJIA JUU WANENGUAJI WANAOVAA NUSU UCHI


Mkurugenzi wa Extra Bongo,Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ naye alikuwepo.Hapa akichangia ambapo alisema kwamba, tatizo la wanamuziki wa dansi wana wivu uliokithiri hivyo kushindwa kuwa na unenguaji wenye kubeba utambulisho wetu.
Mnenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Husna akichangia mada.Aliomba panga la BASATA liwakate wale wanaovaa nusu uchi tu kwani baadhi yao hawavai hivyo.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa kwa pamoja na BASATA na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) na kufanyika kila Jumatatu,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, lazima wadau wa muziki wa dansi wafikirie upya na kubadili mara moja tabia ya kuendekeza maonyesho yanayochafua maadili ya mtanzania.


“Wanenguaji lazima wafikie hatua waseme kwamba, udhalili wa nusu uchi basi tena.Wavae mavazi yenye heshima kama wanavyovaa wale wa kiume” alisema.


Aliongeza kuwa dhana kwamba bila wanenguaji kuvaa nusu uchi maonyesho ya muziki wa dansi hayapati watazamaji na biashara haifanyiki ni uongo na inaonesha jinsi wasanii wa dansi walivyokosa ubunifu wa kuvutia watu kwenye maonyesho yao na badala yake kubaki wakiendeshwa na hisia zisizo za kisanaa.


“Ushindani wa kibiashara ambao unaomfanya msanii kuwa dhalili ili kuvuta watu kwenye maonyesho haukubaliki bali unawafanya wasanii kuwa makapuku na wanaopoteza thamani yao” aliongeza.


Alisisitiza kwamba, BASATA limekuwa likikemea na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya unenguaji wa nusu uchi lakini mabadiliko yamekuwa ni ya muda na baadaye kurudi kwenye udhalilishaji uleule.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...