Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 29, 2010

MISS TANZANIA KUONDOKA KESHO


MKUTANO Mkuu wa Tisa wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), umemchagua Easther Mkwizu akimkabidhi bendera ya taifa Vodacom Miss Tanzania Genevieve Emmanuel tayari kwa safari yake ya kwenda nchini China kushiriki mashindano ya dunia ya Urembo yatakayofanyika Oktoba 31,2010.

Mama mzazi wa Miss Tanzania Genevieve wakiwa na aliyekuwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara Sekta Binafsi nchini Ester Mkwizu na baba yake Emmanuel Mpangala.
Vodacom Miss Tanzania 2010 Ginevieve Emmanuel ametakiwa kulinda heshima yake pamoja na nchi yake awapo katika mashindano ya Miss World kwa kuwa amepewa dhamana ya kuibeba nchi na Amani ya Tanzania.

Nasaha hizo zimetolewa Dar es Salaam leo na Mwenyekiti wa Sekta binafsi, Ester Mkwizu wakati akimkabidhi bendera ya Taifa mrembo huyo tayari kwa safari ya kuelekea China kwenye mashindano ya Dunia ya Urembo ya 'Miss World'.

Ginevieve anatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini China kwa ajili ya Mashindano ya Miss World yatakayofanyika Oktoba 31 mwaka huu, na kushirikisha zaidi ya warembo 120 kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo jana mrembo huyo aliagwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Herman Mwansoko na MKurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Emmanuel Olenaiko pamoja na viongozi mbalimbali.

Ginevieve ametakiwa kuwa jasiri na kupita kifua mbele, mbele ya warembo wengine wote wanaoshiriki mashindano hayo kwa kuwa anavigezo vyote vya kuiwaklisha nchi yake katika mashindano hayo.

"Ginevieve unakwenda kubeba dhamana ya nchi, nenda kifua mbele ukiwa unatoka kwenye nchi ya amani na ulinde heshima yako pamoja na heshima ya nchi yako hapo utafanikiwa, na sisi wanzania tunakuombea dua uweze kutwaa taji la Dunia,"alisema Mkwizu.

Mwenyekiti huyo ameipongeza Kamati ya Miss Tanzania kwa kuendesha mashindano hayo kwa ufanisi mkubwa na kwamba Serikali itaendelea kuwaunga mkono kutokana na Sekta hiyo ya Urermbo kuongeza pato la Taifa kupitia masuala ya utalii na kuenzi pia Utamaduni wa Tanzania.

Naye Ginevieve amewataka watanzania kuondoa hofu juu yake na kwamba hatotishika na wapinzani wake kutokana na maandalizi mazuri ya kisaikolojia aliyoyapata kutoka kwa walezi wake wa Kamati ya Miss Tanzania.

"Nawatoa hofu watanzania ingawa nitashindana na warembo zaidi ya 120 kamwe sitatishika nao, nimeandaliwa vizuri kisaikolojia,"alisema Ginevieve.

Alisema kutokana na fursa hiyo na dhamana aliyopewa na Taifa atahakikisha anatangaza vivutio vya Tanzania kupitia kwa warembo wenzie kutoka nchi mbalimbali pamoja na sekta zote zilizopo nchini.

"kupitia upande wa siasa nitaitangaza Tanzania hasa amani iliyopo na fursa hii nitaitumia bila uoga nawaomba tu watanzania waniombee dua kwani ninajiamini na ninaimani taji la Miss World litatua nchini,"alisema Ginevieve.

Mrembo huyo ataondoka leo na ndege ya Qatar air kwa ajili ya kambi ya Miss World itakayoanza Oktoba mosi mwaka huu na safari yake itapitia Mongolia ambapo atakaa kwa muda wa siku tatu na baada ya hapo atakwenda Shangai ambako pia atakaa kwa siku tatu kisha ataelekea China kabla ya kutua Kusini Sanya kwa mashindano hayo.

Mrembo huyo ni wa 17 kushiriki mashindano ya Miss World tangu kuanzishwa kwa mashindano ya Miss Tanzania 1994 ambapo watanzania wanategemea makubwa kutoka kwake kwa kua ameandaliwa vizuri na walezi wake Kamati ya Miss Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...