Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, September 24, 2010

Peter Mwenda (Buyoya) atimiza miaka 50 (Nusu Karne)


MIMI ni mzaliwa wa kijiji cha Masange wilaya ya Kondoa kabila langu Mrangi ni baba wa watoto watano wa kiume na mke mmoja Elizabert John Mwenda (40) kutoka mkoa wa Mbeya.

Nilifunga ndoa na mke wangu mwaka 1992 katika Kanisa Katoliki Parokia ya St. Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati huo tukiwa na watoto wawili Joseph (Tiria) na John.

Naishi Kitunda, Kivule wilaya ya Ilala nikifanya kazi ya uandishi kampuni ya Business Times katika gazeti la Majira.

Ni muumini wa kanisa Katoliki ambako mwaka huu nilichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Utume Wanaume Katoliki (UWAKA) katika Parokia Mpya ya Kitunda.

Nimepita katika vikwazo vingi vya maisha ikiwemo kuumwa kwa zaidi ya miaka mitatu nikisumbuliwa na magonjwa mbalimbali (siyo UKIMWI) namshukuru Mungu kunivusha katika mitihani hiyo sasa nimepona.

Kilikuwa kipindi kugumu kwa familia, ndugu, majirani, waandishi wenzangu wengine waliniombea nipone, wengine walikata tamaa kwa hali niliyokuwa nayo na wengine walikaa kusubiri kusikia simu ikipigwa kuwapa taarifa ya kifo na wengine kunitangaza nimeathirika.

Wote hao nina wapenda kwa sababu kila unapoishi usifikiri kila mmoja anao upendo wa dhati na wewe,ishi ukijua kuwa nafsi yako ndiyo itakuokoa mbele ya Mungu na

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...