Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 6, 2010

Ghana, Nigeria zashinda Afrika


Lobamba, Ghana
TIMU za taifa za Ghana na Nigeria, zimeibuka na ushindi katika mechi za kusaka tiketi ya kucheza fainali za Matiafa ya Afrika zitakazofanyika 2012.

Mjini Lobamba, Ghana 'Black Stars', timu inayoongoza katika viwango vya ubira wa soka barani Afrika na iliyocheza fainali za Dunia nchini Afrika Kusini na kutinga hatua ya robo fainali, iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Swaziland.

Andre Ayew aliifungia bao la kwanza dakika ya 13, kabla ya Prince Tagoe kuiongezea Ghana bao la pili dakika ya 70 na Hans Sarpei alimaliza bao la tatu dakika ya 81 na kupanda juu ya Sudan katika Kundi I.

Nigeria, ambayo ilitwaa pointi moja katika fainali za Kombe la Dunia, iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Madagascar mjini Calabar, mabao yaliyofungwa na Obafemi Martins dakika ya 19 na Michael Eneramo dakika ya 45.

Lakini, ushindi huo uliisaidia timu hiyo kushika nafasi ya pili katika Kundi B, nyuma ya Guinea iliyoichapa Ethiopia mabao 4-1 mjini Addis Ababa.


Ethiopia walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Umed Ukuri dakika ya 30. Lakini, Ibrahima Yattara aliisawazishia timu yake bao dakika ya 37.

Bao la pili la washindi lilifungwa na Karamoko Cisse dakika ya 60 na Kamil Zayatte alimalizia kufunga bao la nne dakika ya 75 na kuifanya Guinea itoke uwanjani na pointi tatu.

Katika Kundi A, Liberia na Zimbabwe zilitoka sare ya bao 1-1 na kuiacha Cape Verde Islands kuongoza kundi hilo baada ya kuichapa Mali 1-0 bao 1-0, Jumamosi.

Zambia ilikaa juu katika Kundi baada ya kuifunga Comoro mabao 4-0 mjini Lusaka, mechi ambayo ilichezwa baada ya masaa 24 kutokana na kcuhewa kwa waamuzi wa mchezo huo.

Rainford Kalaba aliifungia Zambia bao la kwanza dakika ya tano na Fwayo Tembo aliiongezea bao la pili dakika ya 30 na James Chamanga alifunga bao la tatu dakika ya 40.

Zambia waliingia kipindi cha pili kwa kulisakama lango la wapinzani wao ambapo dakika ya 83, Emmanuel Mayuka aliifungia bao la nne na kuwafanya Chipolopolo watoke uwanjani wakiwa na furaha.

Mechi nyingine katika kundi hilo, Msumbiji na Libya, zilitoka suluhu, mjini Maputo.

Mamadou Niang alifunga mabao matatu mjini Lubumbashi na kuiwezesha Senegal kutoka uwanjani kifua mbele wakiwa na mabao 4-2 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Moussa Sow aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya tatu. Niang aliifungia mabao dakika ya 10na 19, kabla ya bao la penalti alilofungwa dakika ya 68. Wenyeji walijipatia mabao yao kupitia kwa Patou Kabangu dakika ya 44 na 83.

Cameroon wanaongoza Kundi E baada ya kuichapa Mauritius Jumamosi.

Mechi ya Kund F, kati ya Gambia na Namibia mjini Banjul iliahirishwa, wakati Cedric Amissi aliipatia bao timu yake dakika tano na kuzifanya timu hizo za Kundi H, kati ya Burundi na Benin kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mabingwa wa Afrika, Misri ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Sierra Leone mjini Cairo.

Pharaohs walipata bao lao kupitia kwa Alhassan Bangura dakika ya 56, lakini Mahmoud Fathallah aliisaiwazishia timu yake dakika nne baadaye.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...