Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 23, 2010

Zain yaimwagia mapesa Bongo Star Search


KAMPUNI ya simu za mkononi Zain imeingia mkataba kudhamini kwa muda wa miaka mitatu mashindano ya kusaka vipaji kupitia luninga yanayofahamika kama Bongo Star Search yanayoandaliwa na kampuni ya Benchmark kwa pesa za kitanzania Sh, Milioni 100.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Meneja masoko wa Zain Kelvin Twissa alisema lengo la kudhamini mashindano hayo ni kutaka kuinua hali ya maisha ya vijana ili watimize ndoto zao walizojiwekea.

'Sisi kama vinara wa soko la mawasiliano hapa nchini, kushjiriki kwetu katika jitihada hizi za kusaka vipaji zinazoendeshwa na Benchmark ni kutaka kubadili maisha ya vijana kwa kuwapa uelekeo.," alisema Twissa.

Alisema katika kipindi ncho cha miaka mitatu kuanzia sasa kampuni hiyo imepania kuyaboresha mashindano hayo na kuyafanya yaonekane katika kiwango cha kimataifa ili kuijengea sifa Tanzania na eneo lote la Afrika mashariki.

Akifafanua zaidi Twissa alieleza kuwa udhamini huo unalenga kumpa mwanga kila mshiriki na ili ajivunie kushiriki kwake katika mashindano hayo ambayo yanapata umaarufu katika kila kona ya nchi.

Naye Mkurugenzi wa Benchmark Production Rita Paulsen alisema udhamini wa Zain katika mashindano hayo umeleta sura mpya na kuahidi kuvifanyia kazi vigezo vilivyokatika mkataba wao ambapo ameyaomba na kuahidi kuyaongezea msukumo zaidi na uzito.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...