Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, September 23, 2010

Zantel yatoa msaada kituo cha wazeeNa Mwandishi wetu


VITUO vya kulelea wazee vya Zanzibar ambavyo vinahudumiwa na Serikali kupitia mpango wa kitengo cha Ustawi wa Jamii vimepata msaada wa sh. mil.1.5 kutoa Kampuni ya Zantel.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Zantel ilieleza vituo hivyo ambavyo vina wazee 100 vimegawanyika katika sehemu mbili na vinahudumiwa na Walezo Sister Mary Lucy Ngunju na Bw. Khamis Salum ambaye ni mwakilishi wa wazee hao.

Ilieleza makabiziano hayo yalishuhudiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel Zanzibar Bw.Ibrahim Attas na Meneja Masoko Bw.Yusuf Ismail.

Zantel walisaidia kituo hicho mchele, unga ,sukari , maziwa , mafuta ya kupikia, maharage, nguo kama kanga na vingine .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...