Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 29, 2010

MSONDO KUVAMIA KUSINIBENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma imeondoka Dar es Salaam leo kwa ziara ya maonesho matano katika mikoa ya kusini kuanzia Sept 29 mwaka huu baada ya kukaa muda mrefu bila kutembelea kanda hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' (PICHANI) alisema ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuitamulisha albamu yao mpya ya Huna Shukrani.

"Tukiwa huko tutafanya kazi ya kuwapa burudan wapenzi wetu watapata nafasi ya kuona mambo mengi yanayohusu bendi yao kama hayo niliyoyasema.," alisema SUPER D

Alisema wataanza ukumbi wa Bwalo la Maendeleo, Kilwa na Hoteli ya Lindi Oktoba mosi ambapo oktoba 2 watakuwa Brantare Hall na oktoba 3 watakuwa katika ukumbi wa Madeko Masasi, Oktoba 4 Nachingwea na 5 watakuwa Nyongoro Hall, Ruangwa.

SUPER D alisema mbali na utambulisho wa albamu hiyo bendi hiyo pia itatoa fursa kwa wapenzi wake wa mikao hiyo kusikia vibao vipya vya Dawa ya deni kulipa na Lipi Jema vilivyoibwa na wasanii mahiri akiwamo Edo Sanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...