Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 14, 2010

MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU KWA MAKOCHA YANAENDELEA


Kocha wa Makocha kutoka Shirukisho la vyama vya Mpira wa Kikapu Duniani (FIBA) Sanuel Wanjohi (kulia) akitoa mafunzo kwa makocha wa mchezo huo Dar es salaam jana mafunzo hayo yanadhaminiwa na SpriterNYOTA wa zamani wa mpira wa kikapu nchini Marekani Steve Smith anatarajia kuwasili nchini leo kwa ajili ya kwa ajili ya kutoa mafunzo ya siku mbili kwa vijana 30 katika kliniki ya mchezo huo itakayofanyika kesho na keshokutwa katika viwanja vya Leaders Klabu jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Shirikisho la kikapu hapa nchini TBF, kwa kushirikiana na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola kupitia kinywaji chake cha Pepsi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais wa TBF, Phares Maghesa alisema mafunzo hayo yatashirikisha pia makocha mbalimbali wanaoshiriki kozi ya awali ya mchezo huo iliyoanza kufanyika Dar es Salaam jana ili kuwapatia uelewa zaidi.

"Tunatarajia itakuwa ni kliniki yenye mafanikio makubwa ukizingatia mchezaji huyo ana uzoefu na ligi kubwa ya Marekani, NBA na pia aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Marekani ya mpira wa kikapu huo 'The Dream Team, klabu ya Atlanto Hots, Mayami H na zingine nyingi'.," alisema aghesa.

Mafunzo hayo ambayo awali yaliendeshwa na Mtanzania anayecheza ligi ya kikapu ya NBA nchini humo Hasheem Thabeet yanatarajia kushirikisha vijana 30 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara ili kuwawezesha kuujua mchezo huo mapema.

Mbali na hilo kozi ya awali ya makocha ya mpira wa kikapu imeanza kutolewa jana kwa makocha mbalimbli wa mchezo huo ambayo imeandaliwa na Shirikisho la kimataifa la mchezo huo (FIBA).

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...