Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, September 29, 2010

MASHINDANO YA MITUBWI 2010 YAZINDULIWA RASMIKampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa mwaka 2010.

Mashindano hayo ya kupiga kasia, ambayo yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah alisema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika. Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa.

Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyikia Jijini Mwanza tarehe 4 Decemba. Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Kigoma tarehe 9 Octoba, Kagera 23 Octoba, Mwanza 13 Novemba, Mara na Ukerewe 27 Octoba.

Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu mbili za wanaume na moja ya wanawake zitakazoshika nafasi za juu katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Msaidizi wa Bia ya Balimi Edith Bebwa alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo:

Ngazi ya Mikoa Fainali Kuu
Wanaume Wanawake Wanaume Wanawake
Mshindi wa kwanza 700,000 500,000 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 550,000 400,000 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 350,000 250,000 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 300,000 200,000 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 200,000 100,000 400,000 200,000

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki. Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ya aina yake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...