Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 9, 2011

CHAMA CHA NDONDI YA PATA MSAADA YA VIFAA THAMANI YA MIL 5


Na Jamal Zuberi wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo.
DODOMA.
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Dkt. Emannuel Nchimbi ametoa changamoto kwa Taasisi, Mashirika na Watu binasfi nchini kuona umuhimu wa kutoa misaada kwa michezo mingine tofauti na mpira wa miguu.
Akizungumza katika hafla ya kuabidhiwa vifaa vya mchezo wa ngumi vilivyotolewa na Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Serikali za Mitaa L.A.P.F leo mjini Dodoma, Dkt. Nchimbi alisema kuwa wengi wanahisi kuwa mpira wa miguu tu unapewa kipaumbele kwa misaada, tofauti na vyama vya michezo mingine kama vile ngumi na riadha ambazo pia vinahitaji msaada wa kifedha na vifaa.
‘Kwa niaba ya Serikali naishukuru sana L.A.P.F kwa msaada huo wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 5 kwa Chama cha Ngumi nchini BFT ili kufanya maandalizi zaidi kushiriki mashindano ya Ngumi ya nchi za Afrika nchii Msumbiji mwezi ujao.
Ameitaka LAPF kuhakikisha wanaendelea kuweka bajeti ya kuwezesha na kusaidia michezo mingine mwakani .
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw. Don Kida alisema pamoja na kuwa Mfuko huo unajukumu wa kukusanya michango, pia inawajibu kwa jumuia ya wananchi inayoizunguka .
‘Hivyo wanamichizo ni sehemu ya Jumuia za Vijana wetu ambao kama taasisi tunawajibibu wa kusaidia kila inapowezekana hasa wajibu wa kurudisha sehemu ya mafanikio yanayotokana na utendaji wa mfuko huu’, alifafanua Bw. Kida.
Amesema kuwa kwa vifaa hivyo kwa timu ya ndondi ni mfano bora wa kuigwa kwa mashirika,na taasisi mengine ili yaweze kuchangia.
Vifaa ambazo zilitolewa na Mfuko huo ni glovu za mkono, vifaa vya kuhami kichwa, padi za mazoezi, viatu vya mazoezi, track suti, buuta, fulana za mashindao, na vifaa vya mazoezi ya speed ball.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...