Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 27, 2011

Kiduku, Kanga moja kuisindika Melody Idd Mosi


VIKUNDI viwili vya unenguaji vya Kiduku na Kanga Moja vitaisindika
Bendi ya muziki wa taarab nchini East Africa Melody, siku ya idd
mosi katika ukumbi wa Nawina Resorte uliopo Mbagala kuu Dar es
Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana Mratibu wa onesho hilo Zahor
Said, alisema kuwa maandaliziu ya onesho hilo la siku ya Idd mosi
linaendelea kama lilivyopangwa.
Said alisema kuwa burudani hizo zitaanza saa 2:30 ambapo vikundi
hivyo vitaanza kutoa burudani na baadae Melody kutumbuiza mpa
majogoo.
Melody ipo wakongwe mbalimbali wa muziki wa taarabu nchini kama
vile Mwanahawa Ali na Afua Suleiman ambao nyimbo zao zimekuwa
zikitamba sehemu mbalimbali.
Alisema kabla ya onesho hilo la usiku kuanzia saa 9:30 kutakuwa
muziki wa disco toto ambapo watoto watakaocheza vizuri watapata
burudani.
Said alisema zawadi zitakazotolewa ni vifaa vya shule kwa watoto
hao ambapo wataonesha vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...