Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 29, 2011

RAIS DR. JAKAYA KIKWETE ALIPOTEMBELEA BANDA LA MAXCOM AFRICA


Rais wa Tanzania Dr. Kikwete akionyeshwa jinsi mteja anavyoweza kununua umeme kupitia machine ya Maxmalipo na afisa mauzo wa kampuni ya Maxcom Africa Bwana Kulwa Mapigano (kulia) wakati wa kilele cha kongamano la teknolojia ya mawasiliano vijijini (Rural ICT Conference) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akionekana kusisitiza jambo fulani wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maovyesho ya kilele cha kongamano la teknolojia ya mawasiliano vijijini. Kampuni ya Maxcom Africa inatoa huduma za mauzo ya luku, vocha za simu kwa mitandao yote pamoja na TTCL, malipo ya ving’amuzi vya televisheni (DSTV na Startimes), na kutuma na kupokea pesa kwa njia ya M-Pesa, kwa teknolojia ya mtandao ambayo kwa sasa inmawakala wapatao 1,500 nchini Tanzania na Rwanda.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...