Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, August 29, 2011

WATEJA WA VODACOM KUSHINDA ZAIDI YA BILIONI 1 KUPITIA PROMOSHENI MPYA YA MEGA

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, akielezea namna ya kushiriki katika promosheni Mpya ya Mega inayowawezesha wateja wa Kampuni ya Vodacom, kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja, Charity Safford.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu promosheni hiyo Mpya ya Mega inayowawezesha wateja kushiriki na kushinda bila kutozwa fedha.
*******************************************
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza promosheni mpya ya aina yake kwa wateja wake nchi nzima ambao wataweza kujishindia zawadi ya shilingi milioni kumi na moja pamoja na televisheni za kisasa aina ya Samsung LCD mia moja kila siku kwa siku mia moja.

Akitangaza promosheni hiyo iitwayo Mega Promotion jijini Dar es salaam Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba amesema promoheni hiyo ni kubwa kuwahi kuendeshwa na Vodacom tangu ilipofanya mabadiliko makubwa ya kimuono na falsafa mapema mwaka huu yaliyohusisha mabadiliko ya rangi kutoka buluu kuwa nyekundu pamoja na nembo ya kampuni.

Mwamvita amesema promosheni hiyo itadumu kwa siku mia moja kuanzia Agosti 26 hadi Desemab 6 mwaka huu na ili kushinda mteja wa Vodacom atapaswa kujiunga katika shindano la kujibu maswali kupitia simu yake ya mkononi ambapo kupitia majibu ya maswali hayo mteja atakuwa akijikusanyia pointi zitakazoshindanishwa kwenye droo za kila siku.

"Vodacom ni ya kwanza kuleta promosheni ya aina hii, nasema hivi kwa sababu Mega Promosheni inampa mteja fursa ya kuchagua hatua ya ushiriki. Ushiriki wa BURE wa droo za Standard ambapo mteja hujiunga BURE na kuwa na nafasi ya BURE kushinda televisheni moja ya kisasa aina ya Samsung LCD kila siku na hatua nyengine ni ya droo za Premium ambapo mteja atajiunga kwa gharama NAFUU ya shilingi mia tano na hamsini kwa siku kuwania kitita cha shilingi milioni kumi na moja kila siku" Alisema Mwamvita.

Mwamvita ameongeza kuwa ili kushiriki droo ya bure mteja atapaswa kutuma ujumbe mfupi wa neno BURE ama FREE kwenda nambari 15015 na mara moja atapokea swali la kwanza litakaloanza kumpatia pointi ambazo mwisho wa siku zitashindanishwa katika droo ya wazi itakayooneshwa moja kwa moja kupitia televisheni ya ITV kila siku saa moja na dakika hamsini na tano usiku.

Burudani ya aina yake katika promosheni ya Mega ipo katika droo ya Premium ambayo kupitia droo za kila siku inatoa mshindi mmoja wa zawadi ya kitita cha fedha taslimu shilingi milioni kumi na moja.Hata hivyo mteja ana uhuru wa kuchagua kuondoa ushiriki wake katika droo hii wakati wowote.

"Ifahamike kuwa mshiriki wa droo hii ya Premium kwanza lazima ujiunge na hatua ya kwanza ambayo ni ya BURE kuwania televisheni kupitia droo ya Standard na baada ya hapo mteja atakuwa na uamuzi wa kuendelea na hatua ya Premium ambapo mbali na kushiriki na kushinda zawadi ya fedha bado anakuwa na mshiriki wa droo ya Standrd hivyo anaweza kushinda zawadi mbili kwa mpigo"Alifafanua Mwamvita.

Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Promoheni hiyo ya Mega Mkurugenzi wa Mahusiano ya Wateja wa Vodacom Charity Safford amesema Vodacom ina imani kwamba promosheni hiyo itawavutia wateja wake hasa kutokana upekee ilionao.

"Wateja wetu ni kipaumbele chetu cha kwanza kabisa na daima tunajituma kuhakikisha tunawapa huduma bora zaidi kuweza kukidhi mahitaji yatokanayo na shughuli zao za kila siku na kwa mara nyengine tunawaomba watanzania wafurahie hiki tunachowatangazia sasa ambapo kunatoa fursa ya kushinda zawadi kwa kila mmoja aliye tayari kujiunga kwa kulipia au hata yule ambae hayupo tayari kujiunga kwa kulipia lakini anapenda kushinda zawadi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...