Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, August 13, 2011

RAIS MSTAAFU MWINYI AKIKABIDHI MSAADA WA VYAKULA KWA ALBINO
RAIS mstaafu Ali Hassani Mwinyi akimkabidhi msaada wa Chakula, Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Ngozi (Albino) katika Wilaya ya Temeke, Bw. Kassim Kigwe katika hafla fupi iliyofanyika leo (jana) katika shule ya Sekondari Manzese Jijini Dar-Es-Salaam


PICHA ZOTE NA ANNA TITUS -MAELEZO.


RAIS mstaafu Ali Hassani akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu wa Ngozi Tanzania Bi. Ziada Ali Sembo (hayupo picha) wakati alipokuwa akitoa shukrani kwa niaba ya watu wenye ulemavu katika hafla fupi ya kukabidhi chakula cha msaada kwa kundi hilo.


RAIS mstaafu Ali Hassani Mwinyi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika hafla fupi ya kukabidhi chakula cha msaada kwa makundi yasiyojiweza katika jamii. Katika hafla hiyo iliyofanyika leo Dar-Es-Salaam, Rais Mwinyi alikabidhi viroba (vifurushi) 224 vya vyakula vyenye thamani ya Tsh Milioni 15.

RAIS mstaafu Ali Hassani Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Rehema, Bw. Abdi Adam wakati alipokuwa akitoa risala fupi ya taasisi hiyo. Watatu kutoka kwa Rais mstaafu ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Bi. Alshaymaa Kweir na anayemfuatia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Walemavu wa Ngozi Tanznia, Bi. Ziada Ali Sembo.

http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...