Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 30, 2011

TTCL YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO

Afisa Mkuu wa Fedha wa kampuni ya TTCL Mrisho Shaban Mrisho akikabidhi msaada wa chakula va vitu mbalimbali kwa Juma Lukinga mwalimu mkuu wa Shule ya uhuru Mchanganiko leo jijini Dar es salaam, Kampuni ya TTCL imetoa msaada huo wa vyakula na vifaa vingine wenye thamani ya shilingi milioni 3.5 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El-Fitr inayotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanizl leo kutegemea na mwezi utakavyoandama. Kulia katikati ni Mfaume Juma darasa la tano na kushoto ni Maliki Braitoni darasa la tano wanafunzi wa shule hiyo wenye ulemavu wa macho, vyakula vilivyotolewa ni pamoja na Mchele, Maharage, Sukari, Unga wa ngano, Unga wa Sembe, Mafuta ya Kula na Sabuni
Hivi ni baadhi ya vyakula vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa watoto wa shule ya Uhuru Mchanganyika.
Mrisho Shaban Mrisho Afisa Mkuu wa Fedha TTCL akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Uhuru Mchanganyika Maliki Braiton na Mfaume Juma wenye ulemavu wa macho mara baada ya kupokea msaada wa chakula leo, kulia anayeshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Juma Lukinga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...