Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, August 30, 2011

MABONDIA WA ZAMANI WATAKIWA KUFADHILI NGUMI


BINGWA wa Mchezo wa kick Boxing nchini Japhet Kaseba amewaomba Mabondia wakubwa kuhakikisha wanaweka na kuchangia fedha zitakazo kuwa zikitolewa kuchangia vyama vya michezo nchini wikiwemo RT na BFT.

Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili leo kwa njia ya simu Gwiji huyo wa Mapigano amesema itakuwa ni jambo zuri kwa mabondia wakubwa kutenga fedha ili kuchangia vyama vya michezo mbali mbali nchini wikiwemo vya Ngumi za ridhaa na riadha badala ya kutegemea nguvu ya serikali tu.

"Sifikili kama tukijaribu tutashindwa japo kwa kiasi kidogo kidogo tuweke mazoea ya kuchangia vyama hivi kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla kuliko kutegemea serikali tu"alisema Kaseba.

Hata hivyo Kaseba amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mashindano ya All African Games ambayo yanatarajia kurindima hivi karibuni nchini Msumbiji yupo mbioni kuandaa filamu itakayo kuwa ikielezea umuhimu wa kuwekeza katika michezo.

"Lengo la hii filamu ni kujaribu kuwapa hamasa wadau kuwekeza na kuchangia michezo ila pia nataka kuwashirikisha wanamichezo mbali mbali"alisema Kaseba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...