Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 14, 2011

WANAWAKE KUAMASISHA NGUMI IDI PILI MORO


MABONDIA Asha Abubakar na Fadhila Adam wanatarajia kudundana katika pambano la kuhamasisha ngumi kwa wanawake litakalofanyika siku ya Idd pili katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.

Pambano hilo litakuwa ni miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya mabondia wa ngumi za kulipwa Fransic Cheka na Mada Maugo.

Pambano hilo la ubingwa wa UBO linatarajia kuwa katika raundi 10 uzito wa Kg 72 huku likisimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa (PST).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Promota wa ngumi hizo Kaike Siraju alisema, pambano hilo la kuhamasisha litakuwa la raundi 6 huku likiwa katika uzito wa kg 52 ambalo litakuwa ni moja ya pambano la kivutio siku hiyo.

"Wanawake ni wachache sana wanaoshiriki katika mchezo huu hivyo ni naimani watu watapata burudani ya kutosha kutoka kwa wadada hao," alisema kaike.

Alisema, kwa upande wa Maugo na Cheka kila bondia anaendelea kujifua katika gym yake tayari kwa kusubiri siku hiyo ambapo maandalizi yanaendelea.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo hapo uwanjani na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...