Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 19, 2011

TTCL YASAINI MKATABA WA KUUZA VOCHA NA MAXCOM AFRICA

TTCL imeingia mkataba na kampuni ya MAXCOM AFRICA uwakala wa kuuza voucher za internet na simu za kawaida kwa njia ya mtandao (Electronic Voucher
Distribution).

Wanachofanya wao ni kuwapa mawakala (agents) wao katika maeneo mbalimbali vifaa vya electroniki (Electronic Devices) vyenye uwezo wa kutoa vocher hizo.

Kwa maana nyingine ni kwamba hawatauza kadi za kawaida za TTCL kama ilivyo sasa, isipokuwa namba za kuongezea muda wa maongezi/internet (airtime PINs) zitakazochapishwa (printed) kwenye karatasi kutoka katika machine hizo.

Maxcom Africa wana mpango wa kupeleka huduma hii katika mikoa yote ndani ya nchi. Hili linatuongeze sisi TTCL matumaini zaidi katika kuboresha huduma kwa wateja wetu.

Mkurugenzi wa TTCL Said Amri Said ametoa angalizo kuwa pamoja na kuingia mkataba huu, bado vituo vyetu vya huduma kwa wateja na mawakala wetu wataendelea kuuza kadi/voucher kama kawaida.

Technologia hii ya kuuza kadi kwa mtandao inawawezesha kutoa huduma katika vituo vingi zaidi na maeneo tofauti hivyo kuwafikia wateja wetu katika maeneo mengi zaidi.

TTCL inaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika kufanikisha utoaji wa huduma hii ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wateja pale itakapohitajika.

TTCL inayofurahia zaidi kwani ushiriki wa Maxcom katika kusambaza vocha zao kunatuhakikishia huduma bora, ya uhakika na ya karibu kwa wateja wake kwa muda mwingi zaidi.

Uzoefu wao katika biashara hii unwapa faraja zaidi kwani kunawahakikishia upatikanaji wa vocha za TTCL kupitia mtandao wa kuaminika. Mkurugenzi huyo amewaomba wateja wao wavitumie vituo vya Maxcom na wawe huru kuuliza mahali pote waonapo alama ya Maxcom na TTCL.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...