Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 15, 2012

AFA AKIANGALIA MECHI YA YANGA NA RUVU SHOOTING

FUNDI seremala wa Kiwanda cha Alminium Africa, Erasto Kandeo (41), amefariki baada ya kudondoka katika Uwanja wa Taifa alipokuwa akiangalia mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyofanyika Februari 12 mwaka huu.

Kamanda wa Polisi Temeke, David Misiime alisema taarifa kutoka kwa kaka wa marehemu, Richard Kandeo (46), alisema kuwa mdogo wake alidondoka ghafla saa 11.00 jioni baada ya kupata mshtuko akiwa anaangalia mechi hiyo.

Alisema baada ya kuanguka Erasto alikimbizwa katika Hospitali ya Temeke na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini alifariki dunia akiwa njiani.

Kamanda Misiime alisema maiti ya Erasto imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...