Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, February 21, 2012

Collapse all Expand all Print all In new window Wanahabari washindana kuonja ladha ya bia za TBL Mbeya

Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mbeya, Calvin Martine akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya, kuhusu uzalishaji wa bia walipotembelea kiwanda hicho, mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wanahabari wakichungulia sehemu inayotumika kupikia bia katika kiwanda cha bia cha Mbeya.

Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakitembelea kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kilichopo Iyunga jijini humo mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya waandishi wa habari wa jijini Mbeya wakishindana kutambua ladha ya bia za kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akimkabidhi katoni ya bia aina ya Castle Lager, mwandishi wa habari wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Steve Jonas ambaye alikuwa ni mshindi wa pili kati ya washindi watatu waliofanikiwa kubaini ladha halisi ya bia zinazotengenezwa na kampuni hiyo Jijini Mbeya mwishoni mwa wiki.

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari Leo Joachim Nyambo akipokea zawadi ya katoni ya Bia aina ya Ndovu kutoka kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi baada ya kuibuka mshindi wa kubaini ladha halisi ya aina ya vileo vinavyotengenezwa na kampuni ya Bia ya TBL.Mashindano hayo yaliyohusisha wannahabari wa mkoa huo yalifanyika mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...