Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 27, 2012

Waziri Tibaijuka akabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya NBC Lady Captains’’ Trophy 2011.Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi aliyepiga umbali mkubwa zaidi, Vivienne Mwaulambo wa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011 katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale ambaye benki yao ilidhamini mashindano hayo.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi wa jumla wa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011, Halima Makame yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC Katika Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia) akikabidhi kikombe kwa mshindi wa tatu wa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011, Violet Peter katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam juzi.

Mmoja wa viongozi wa DGC kitengo cha gofu ya wanawake, Joyce Srvarva (kulia) akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale kwa kutambua mchango wa benki hiyo kufanikisha mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011 katika viwanja hivyo juzi

Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka (wa pili kulia) akipiga picha ya kumbukumbu na viongozi wa kitengo cha gofu ya wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Gofu ya Lady Captains’ Trophy 2011 yaliyodhaminiwa na NBC katika viwanja hivyo juzi. (Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NBC, Mwinda Kiula-Mfugale)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...