Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 29, 2012

TPBC KUANZISHA TAASISI YA RASHID MATUMLA SPORTS ACADEMY


Katika juhudi za kuwaenzi wanamichezo walioliletea sifa kubwa taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) iko kwenye mchakato wa kuanzisha Taasisi ya Michezo ya Rashid Matumla (Rashid Matumla Sports Academy) ya kuibua vipaji vya vijana wanaochipukia katika michezo hususan ngumi.


Huu ni mkakati wa kumwandaa bingwa wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (Rashid Matumla) kustaafu ngumi ili aweze kutumia kipaji chake cha ngumi kuendeleza vijana.


TPBC inajivunia historia nzuri ya Rashid Matumla kwa kuwa bondia wa kwanza Tanzania kuwa bingwa wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) pamoja na sifa kemkem alizoliletea taifa hili kipindi hiki chote anachopigana ngumi. Tunapenda kuutangazia umma kuwa tunamwandalia Rashid Matumla mazingira mazuri ya kustaafu ngumi.


Katika taasisi hiyo ya Rashid Matumla Sports Academy, Rashid atakuwa ndiye Rais na atakuwa analipwa mshahara kama mwajiriwa kwa kipindi chote cha uhai wa taasisi hiyo na kumfanya aweze kujipatia ajira ya kudumu wakati hachezi tena ngumi. Huu ni moja ya mikakati ya TPBC kuhakikisha kuwa mabondia wake walioiletea nchi hii heshima kubwa wanaenziwa kwa kuandaliwa maisha mazuri wanapostaafu ngumi!


Ni lazima kama taifa tuwajali wale wote wanaolipigania taifa hili na tutaendelea pia kuandaa mazingira mengine ya kuwawezesha waishi vizuri na kuheshimiwa daina ili kuleta changamoto kwa wengine ili nao wapigane kufa na kupona kuliletea sifa taifa letu katika michezo.


Taasisi hii itazinduliwa rasmi wakati wa mpambano wa Rashid Matumla na Vitaly Shemetov bondia anayetoka Urusi litakalofanyika mjini Moshi tarehe 22nd Juni na kuhudhuriwa na Mcheza sinema maarufu wa Marekani, Deidre Lorenz wa sinema maarufu ya Santorini Blue. Mcheza sinema huyo atakuwepo nchini kwa ajili ya kukimbia mbio za Marie Frances Mt. Kilimanjaro Marathon kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika zikazofanyika tarehe 24 Juni mwaka huu kuanzia Moshi Club.Taasisi ya Rashid Matumla Sports Academy ambayo itakuwa inafanya kazi nchi nzima itajumuisha pia bingwa mwingine wa zamani wa dunia aliyetambuliwa na Umoja wa Ngumi wa Dunia (WBU) Magoma Shaban. Hawa wote watakuwa waajiriwa wa taasisi ya Rashid Matumla Sports Academy wakifanya kazi za kuibua vipaji kwa vijana Tanzania nzima!No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...