Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 29, 2012

SIMBA KUZINDUA TELEVISHENI YAKE

Ezekiel Kamwaga akionyesha kadi ya kiingilio kwenye hafla hiyo

Klabu kongwe ya soka Tanzania, Simba Sports Club, imetangaza kuzindua Tv yake itakayokwenda kwa jina Simba TV.


Akitangaza leo kwenye makao makuu ya Klabu hiyo, mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa 'Mnyama' huyo Ezekiel Kamwaga amesema uzinduzi wa Luninga hiyo unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii katika hoteli ya JB Belmont katika jengo la Benjamin Mkapa katikati ya jiji la Dar es Salaam.


Kamwaga amesema, Simba Tv itakuwa ikirushwa kupitia kituo cha Clouds Tv na kwamba wakati wa uzinduzi kutakuwa na burudani mbalimbali hukuzikionyeshwa documentary maalum inayohusu klabu hiyo.


"Hafla hii itakuwa ni kwa waalikwa huku wengine watakaopenda kuhudhuria watapaswa kulipa shilingi 70,000.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...