Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 17, 2012

Usajili wa Watunzaji (Custodians) na Wawekezaji (Fund Managers)Tunapenda kuutaarifu Umma kwamba Mamlaka itaanza kusajili Watunzaji (Custodians) na Wawekezaji( Fund Managers) kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 5 (1)(a) cha Sheria ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii. Usajili huo utaanza tarehe 20 Machi 2012,

Hivyo Mamlaka inaalika Kampuni zenye sifa za kuwa Watunzaji na Wawekezaji ili watume maombi ya kujiandikisha.

Kwa Watunzaji na Wawekezaji ambao tayari wamesajiliwa katika Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) wanaombwa kuambatanisha kivuli cha cheti cha usajili kikionesha pamoja na mambo mengine namba ya Usajili.

Angalizo: Taratibu za Uandikishaji wa Mifuko ya Hiari (Supplementary Schemes/Occupational Schemes) zitafuata baadae .

Kwa maelezo zaidi juu ya kujisajili tafadhali tembelea tovuti yetu: www.ssra.go.tz au wasiliana na;

Mkurugenzi Mkuu


Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii

Jengo la Alfa, New Bagamoyo Road

S.L.P 31846, Dar es Salaam

Simu: +2559(22) 2761683-4/2761689

Nukushi +255(22) 2761681

Barua pepe: info@ssra.go.tz

Tovuti: www.ssra.go.tz


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...