Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 8, 2012

Waomba Tamasha la Pasaka kufanyika uwanjani


KAPSHENI: Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama akiteta jambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.




MWENYEKITI wa tamasha la Pasaka, Alex Msama, amesema wadau wengi wanataka tamasha la mwaka lifanyike katika ukumbi mkubwa ama sehemu yenye nafasi ya kutosha kama uwanja wa mpira wa miguu.

Akizungumza na Dar es Salaam jana, Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo, alisema walipokea maombi kutoka kwa wadau wakitaka tamasha hilo lifanyike kwenye uwanja wa mpira wa miguu, hivyo kamati yake itakutana na kujadili suala hilo.

"Kila kitu kina mpangilio wake na kinafanyika kwa kufuata vikao vya kamati, tutakaa na wenzangu na kulishughulikia suala hilo," alisema.

Msama alisema, tamasha la mwaka huu linatarajiwa kuwa na waimbaji wachache nyota ambao watalifikisha neno la Mungu vizuri kwa njia ya nyimbo.

Alisema tangu kumalizika kwa tamasha la mwaka jana lililofanyika Diamond Jubilee, ambalo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete, wadau wengi wametuma maoni ya kutaka mwaka huu lifanyike katika sehemu kubwa.

"Maoni tuliyopata kutoka kwa wadau wa nyimbo za Injili yametupa kazi kubwa sana, tutayafanyia kazi haraka," alisema.

Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha Aprili 8 na 9.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...