Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kuwasaidia kupata huduma bora kwa hakina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5,hususani maeneo ya vijijini.
Naibu Mkurugenzi Mkuu bwn. Hamis Mdee akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu kuhusu namna ambavyo mradi huo unavyotekelezeka kwa kasi Mkoani Tanga kabla ya kuanza kwa mkutano wa uzinduzi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Imanuel Humba, kushoto ni Mwakilishi wa KFW, Dk. Kai Gesing kabla ya uzinduzi wa mradi huo, ambao huko chini ya usimamizi wa NHIF kwa Mikoa ya Tanga na Mbeya kwa majaribio.
Pichani mmoja wa wanufaika wa mradi KFW akipokea kitambulisho cha kupata huduma za afya kwa niaba ya wenzake 600 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi Chiku Galawa, wanaoshuhudia pembeni kulia ni Mkurugenzi mkuu wa NHIF Bw. Imanuel Humba na Dr. Sweya ambaye ni meneja wa Mradi kutoka NHIF.
No comments:
Post a Comment