Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 16, 2012

Tamasha la Pasaka kurindima Kirumba aprili 9 baada ya Dar es salaam






Mwimbaji wa muziki wa injili Solomon Mukubwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiimba katika mija ya tamasha la Pasaka, lililofanyika mwaka jana kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Na Mwandishi Wetu TAMASHA la Pasaka litakalofanyika Dar es Salaam, Aprili 8 mwaka huu, pia limepangwa kufanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Aprili 9 mwaka huu. Awali, tamasha hilo lilipangwa kufanyika Dar es Salaam kisha Jumatatu ya Pasaka lifanyike Arusha, lakini sasa litafanyika Mwanza siku hiyo. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na maombi ya wadau mbalimbali. Msama alisema tamasha la Pasaka litapambwa na waimbaji nguli wa nyimbo za kumsifu Mungu kutoka nchini na nje ya nchi kama Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, na akabainisha muda si mrefu wataanza kuwatangaza baada ya kufikia makubaliano. Tamasha la Pasaka la mwaka huu lina malengo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima, kuwasaidia mitaji ya biashara wajane wasiojiweza na wengine wenye mahitaji katika jamii. "Tutaendelea kupanua wigo zaidi wa tamasha la Pasaka mwaka huu kwa vile litashirikisha wasanii kutoka nchi kadhaa za Afrika. "Tumeboresha mambo mengi kuliko miaka iliyopita, waimbaji mwaka huu watakuwa si wengi sana wakiwamo wa kutoka mataifa mengine ya Afrika... hiyo yote tumefanya ili kukidhi matakwa ya wapenzi wa muziki wa injili na wote wapate nafasi nzuri ya kuburudisha," alisema Msama. Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili akiwa mwasisi wa matamasha ya injili nchini, alisema lengo la kuwajumuisha wasanii hao ni kutaka kulifanya tamasha hilo kuwa tofauti na miaka mingine. Alisema tamasha hilo litakuwa na kiingilio cha chini zaidi (kitatangazwa baadaye), ili kila mmoja ahudhurie na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu. "Waimbaji wengi maarufu wa muziki wa injili watakuwepo, tumejipanga vizuri kuhakiksha tamasha hili linakuwa gumzo kila mahali," alisema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...