Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 17, 2012

SWEETHEART CREM YASHEREHEKEA SIKU YA VALENTINE KWA KISHINDO


Mwanamke ambaye jina lake halikupatikana mara moja akipokea zawadi ya maua,kadi na chupa ya kipodozi cha sweetheart wakati wa promosheni ya bidhaa hiyo iliyofanyika mjini Arusha siku ya sikuu ya wapendanao.Vijana wakiongea na mteja kuhusu promosheni ya Sweetheart Cream katika promosheni hiyo iliyoandaliwa jijini Mwanza siku ya wapendanao.


---

Krimu ya Sweetheart yatikisa majiji ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha siku ya Valentine ambapo wanaume watanashati walibeba mabango yaliyosema piga honi kama unahitaji krimu ya Sweetheart.Katika makutano ya Morocco jijini Dar es Salaam kulikuwa na mwitikio mkubwa ambapo watu wengi walipiga honi kuhitaji krimu na wadada warembo waliwapatia krimu hiyo. Makutano mengine yaliyolengwa ni Ubungo na Chang’ombe. Krimu nyingi zilichukuliwa jijini mwanza kama tunavyojua wasukuma walikuwa na shauku ya kupata krimu hii kwasababu ilikuwa ni mara ya kwanza kwao. Makutano yaliyofana zaidi ni mabatini. Pia kulikuwa na promosheni hii katika jiji la Arusha.Meneja wa promosheni wa Sweetheart Cream alisema wakati anahojiwa na waandishi wa habari kwamba Sweetheart Cream ni cream ambayo haina madhara na kwa leo siku ya wapendanao wameweza kugawa kadi pamoja na uwa na wateja wameweza kuitumia Sweetheart cream. Pia Neema aliongezea kusema kwamba hii creamu ya Sweetheart ni nzuri kuliko zingine kwasababu ina kemikali inayoitwa Dimethocone nah ii inalinda ngozi yako dhidi ya jua.Aliongezea kwamba katika supermarket ya Uchumi wameweza kuwa na mteja ambaye alinunua Sweetheart Cream aina ya Carott na motto wake alikuwa anamsisitizia acheze kwenye draw kusudi aweze kupata nafasi ya kwenda kula kwenye mgahawa maarufu.Siku ya Valentine katika supermarket ya TSN Krimu ya Sweetheart aina ya Carrot ilinunuliwa zaidi na wateja waliopenda sana muonekano mpya wa pakiti za krimu ya Sweetheart. Katika supermarket ya Uchumi, wateja waliendelea kuulizia kuhusu kemikali zinazolinda ngozi dhidi ya jua. Kulikuwa na watoto waliokuwa wakiwaomba wazazi wao kuwa nunulia Sweetheart ya gramu 100 ili washiriki katika michoro ambayo iliwapa nafasi wazazi wao ya kupata chakula kwenye moja kati ya migahawa mikubwa jijini.Kulikuwa na promosheni ya Sweetheart iliyokuwa ikiendelea kwenye radio ya Clouds FM ikielezea aina na ubora wa matumizi ya krimu za Sweetheart kwa wasililizaji. Radio zinaendela kuwaelezea wasikilizaji ubora na matumizi ya krimu za Sweetheart na kutoa zawadi mbalimbali kwa wasikilizaji washiriki.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...