Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 29, 2012

RATIBA YA SANDTON SOUND BAND KWA WIKI

Sandton Sound Band ilianzishwa mwaka 2002 ikijulikana sana kwa jina la Bendi ya Manzese, Wana Bandika Bandua, Watoto wa Manzese, nk. Bendi ina jumla ya Album 2. Majina ya Album hizo ni Sandton Tunakuja, Kisokolokwinyo, na ya tatu ipo njiani . Tuna furaha kusema kwamba bendi mpaka kufikia mwaka 2012 imetimiza miaka 10. Si jambo rahisi. Mwaka huu 2012 tutaadhimisha miaka 10 ya bendi kwa kufanya show kubwa tukishirikiana na bendi/taarabu zingine.
Ratiba ya Bendi ni kama Ifuatavyo:
  • Kila Alhamisi bendi inapiga Manzese Tip top uwanja wa Nyumbani kwenye Bar ya Sandton City

  • Kila Ijumaa Bendi inapiga Bar mpya pale Manzese Darajani

  • Kila jumamosi Bendi inapiga Anamwana pale Kimara Rombo

  • Na kila jumapili bendi inapiga Mbezi Kimara stendi ya Kibanda cha Mkaa


Tunawashukuru wadau wetu wote. Karibuni SANDTON SOUND BAND


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...