Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, February 23, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA CHA SAAFI CHA SUMBAWANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu uchinjaji wa Ng’ombe na matayarisho yake hadi kufikia nyama kamili kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya, kilichopo Sumbawanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu matayarisho na ufungaji wa nyama katika mifuko tayari kwa kuuzwa kwa wateja kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha Nyama cha Saafi, Dkt. Engelbert Bilashoboka, wakati alipotembelelea Kiwanda hicho cha Mtazania Mzawa, Dkt. Mzindakaya, kilichopo Sumbawanga, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Katavi na Rukwa jana.


Ziara ya kutembelea shughuli za kiwanda hicho zikiendelea.


Ngombe akiandaliwa tayari kwa kuchinjwa kwa kutumia mashine ya umeme.


Mheshimiwa akiangalia moja kati ya Ng'ombe akichinjwa kwa mashine ya umeme kiwandani hapo.


Ng'ombe akiwa tayari amekwisha kula kisu ili kumwa damu baada ya kupigwa shoti ya umeme na kukusanya damu akiwa katika mashine hiyo inayomchinja, ambapo hapa kazi ya mshika kisu ni kukata ngozi tu ili kumwaga damu.


Picha ya pamoja ya kumbukumbu baada ya kumaliza ziara hiyo

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...