Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 13, 2012

TFDA YATEKETEZA VIPODOZI NA MADAWA YENYE THAMANI YA MILIONI 20.


NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA
MAMLAKA ya chakula na dawa mkoa wa Arusha (TFDA) imeteketeza bidhaa vikiwemo vipodozi mbalimbali visivyofaa kwa matumizi ya binadamu ,zilizokuwa kwenye mzunguko wa kibiashara zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20.
Bidhaa hizo ni pamoja na vyakula mbalimbali vilivyoisha muda wake, vipodozi vilivyopigwa marufuku , madawa bandia ya binadamu na bidhaa zisizosajiliwa.
Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi mara baada ya kuteketeza bidhaa hizo, katika dampo la manispaa lililopo Muriet jijini hapa , Mkaguzi wa dawa wa TFDA kanda ya kaskazini, Bw Elia Nyeura alisema kuwa,kupatikana kwa bidhaa hizo ni kutokana na operesheni waliyoifanya kati ya januari 3 hadi 25 mwaka huu,katika wilaya tatu zilizopo mkoani Arusha.
Alifafanua ya kuwa operesheni hiyo imefanyika katika wilaya tatu ambazo ni Arusha mjini,Arumeru na karatu na kwamba kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo walifanyatathimini na kujiridhisha kuwa maeneo hayo yamekuwa kichaka cha bidhaa hizo zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.
Aidha alisema jumla ya vituo vya afya na maduka ya madawa ya binadamu 131 wameyafanyia ukaguzi, pamoja na maduka ya vyakula 60 yaliyopo katika wilaya hizo yalikaguliwa.
Aliongeza kuwa miongozi mwa dawa zilizoteketezwa ni pamoja na dawa za kuongeza makalio aina mbalimbali , kwa upande wa baadhi ya vipodozi vilivyozuiwa na serikali ni pamoja ,G$ G Cream,Carottene,Bio Carote,Carolight,Mekako ,Maxi light na vinginevyo vingi ambapo alifafanua kuwa vipodozi hivyo vimegundulika kutengenezwa na madini hatari , aina ya Hyroguinine,Steroids,Bithionol,mercury (Zebeki).
Alisema athali kubwa kwa matumizi wa vipodozi hivyo ni pamoja na kupatwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi, akina mama kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na kupatwa na athari ya uharibifu wa ini na figo na kwamba athari hizo humpata mtumiaji kwa muda mrefu bila yeye kujitambua.
Hata hivyo amewataka wafanyabaishara kuwa makini na bidhaa bandia nazile zilizoisha muda wake ,kadhalika kuwacha kuingiza nchini bidhaa zilizopigwa marufuku na serikali ,kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria na taratibu za nchi na wahusika watachukuliwa hatua.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...