Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 17, 2012

Airtel Tanzania yazindua Promosheni Mpya ya 'Nani Mkali'


Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
• Mamia kushinda fedha taslimu
• Zaidi ya milioni 200 kuzawadiwa

15, Februari 2012 Siku moja baada ya Valentine Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imezindua promosheni mpya itakayowawezesha wateja wake kujishindia mamilioni ya fedha taslimu ijulikanayo kama “Nani
Mkali”

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando (pichani kati) alisema “ leo Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na kushindafedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi. Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, kila siku kutakua na mshindi wa milioni moja,kila wiki milioni tatu na kila mwezi milioni thelathini(30).

Kuhusu jinsi ya kujiunga na “Nani Mkali”, afisa bidhaa wa Airtel bi Alice Paulsen alisema,”tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru katika promosheni hii mteja anatakiwa kuandika neno

“Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa ili kujiunga. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.

Promosheni hii pia itatoa fursa kwa wateja kuchagua lugha wanayotaka kwa kutuma neno “swa” kwa Kiswahili au “eng” kwa lugha ya kiingereza kwenda namba 15595 Kujua alama ulizonazo au point mteja wetu atatakia kutuma neno “point” au “alama” kupatiwa pointi alizojikusanyia. Kujiondoa mteja atatakiwa kutuma neno “cancel’ au “stop” kujindoa kwenye promosheni.

Akitoa ufafanuzi zaidi Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando aliongeza kwa kusema promosheni ya “Nani Mkali” inazinduliwa leo ikiwa bado promosheni yetu kubwa ya Mzuka wa Airtel inaendelea ambapo wateja wanajishindi simu,muda wa maongezi pamoja na pesa taslimu zaidi ya shilingi milioni 50.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...