Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, February 27, 2012

AIRTEL YAWAZAWADIA WASHINDI WA “NANI MKALI” PROMOSHENI· Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki wazawadi


27, Februari 2012 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewazawadia washindi wa wiki ya kwanza ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo washindi wa kila siku wamekabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi wa wiki ameondoka na shilingi milioni tatu. washindi hao wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Mwanza, Tanga, Mbeya, Arusha na Dar es Saalam


Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali. Na leo napenda kuchukua fulsa hii kuwatangaza washindi wa wiki ya kwanza ambao ni Bw Daniel Mshana , Dr. Hetal Anthan na Albogast Oiso wa Dar es saalam, wengine ni Said Seif wa Mwanza,Junior Pesambili wa Arusha na Abdi Ibrahim Mohamed wa Muheza Tanga hawa walijishindia million moja kila mmoja na ambapo bwana Abdi Ibrahim zaidi ya kuwa mshinidi wa siku ameibuka kuwa mshindi wa wiki na kuondoka na pesa taslim shilling million tatu”.


Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Matinde


kujiunga na “Nani Mkali”, mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na

1 comment:

  1. I TOO I BELIEVE I WILL GET SOMETHING LIKE DA MUHEZA MAN
    !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...