Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, February 8, 2012

MFANYABIASHARA MWANZA AMWAGA MISAADA KUSAIDIA ELIMU, USALA WA RAIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Nwanza Huduma Ltd ya jijini Mwanza, Zulfikar Nanji katika shati la drafti rangi ya blue) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamanda Barlow (katikati) na maofisa wengine wa polisi, baada ya kukabidhi matairi yenye thamani ya sh. milioni 20 kwa ajili ya magari ya polisi. Hafla hiyo ilifanyika jijini mwanza mwezi huu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwanza Huduma Ltd, Zulfikar Nanji akimkabidhi saruji mifuko 400, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara mapema mwezi huu kwa ajili ya serikali ya mkoa huo kujenga madarasa ya sekondari. Baadaye Nape akikabidhi Saruji hiyo kwa Mkuu wa mkoa huo John Tupa (kushoto).
HABARI KAMILI
NanjiMkurugenzi Mtendaji wa Mwanza Huduma Ltd, Zulfikar Nanji mwanzoni mwa mwezi huu alionyesha moyo wa uzalendo kwa kuisaidia serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutoa michango kwa ajili ya kusaidia sekta ya Usalama wa Rais na mali zao na sekta ya elimu mkoani Mwanza.


Msaada wake wa kwanza ambao mtayarishaji wa mtandao huu aliushuhudia ni mfanyabiashara huyo kuwapa Polisi mkoa wa Mwanza matairi yenye thamani ya jumla ya sh. milioni 20 kwa ajili ya karandinga sita na Landcruiser kumi.


Akikabidhi matairi hayo, Nanji alisema ameamua kulisaidia jeshi la polisi mkoani humo ili kuliongezea uwezo katika utendaji kazi zake kwa kuwa amefahamu kuwa polisi inahitaji magari yenye matairi yaliyo bora ili kuweza kufanya kwa uhakika operesheni zake za kuhakikisha usalama wa rais na mali zao vinaimarika.


Msaada mwingine ni kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya kuuwezesha mkoa wa Mara kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa ambao umesababisha kiasi cha watoto 6486 kuanza masomo ya kidato cha kwanza licha ya kwamba wamechaguliwa kujiunga sekondari.


Nanji alikabidhi mifuko hiyo ya saruji kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika halfa iliyofanyika kwenye Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara mjini Musoma.


Baada ya kukabidhiwa Nape naye alikabidhi saruji hiyo kwa mkuu wa mkoa huo, John Tupa ambaye alisema itasaidia kujenga madarasa haraka iwezekanavyo na kuhakikisha kwamba hadi mwezi ujao wa Machi watoto wanaanza masomo.http://bashir-nkoromo.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...