Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, February 17, 2012

Chisora atamba kumtwanga Vitali
kwa KO
LONDON, Uingereza
DERECK Chisora ametamba kuwa anaweza kutwaa ubinga wa dunia kwa kuwa hatabiriki na kwamba hajui ni kitu gani kitatokea, umesema mtandao wa The Sun.
Del Boy atapambana na bingwa mtetezi wa WBC, Vitali Klitschko mjini Munich kesho Jumamosi ambapo ameahidi kuibuka na ushindi wa KO katika raundi ya nane.
Chisora anatumaini kuwa atafuata nyayo za mpiganaji mahiri wa zamani wa Uingereza, Lennox Lewis ambaye limtwanga Vitali mwenye urefu wa futi sita na ichi saba.
Alisema: " Ninaahidi kuwa ninasonga mbe kuanzia kengele ya kwanza, katika raundi ya nane atakwua mepigwa kwa KO.
"Kwanini raundi ya nane 8? ninaipenda namba nane kwa ubora . Timu ya Klitschko hainipendi kwa kuwa ni sitabiriki na sugu. Ni mwisho wa Vitali, ninaahidi."
Chisora mwenye umri wa miaka 28, yuko fiti sana kwa jili ya kupambana na mpinzani wake mwenye umri wa miaka 40, Klitschko ambaye ni kaka wa Wladimir.
Vitali, alipigwa na Lewis mwaka 2003, lakini alisema: "Waingereza wanapenda sana kuchonga. Nitamfundisha somo. Hakuna mtu wa kunizuia."

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...