Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein
Rashid ‘Hussen Machozi’ amesema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa
kibao chake kipya ambacho bado hajakipatia jina.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam alisema kutokana na ubora wa wimbo huo anapata tabu kujua aupe jina
gani na anaimani mwisho wa mwezi huu utaanza kusikika redioni.
“Unajua kazi ikiwa freshi inakua tabu kutafuta
jina la wimbo, hivyo nipo kwenye mchakato wa kutafuta ikibidi nitaomba ushauri
kwa wasanii wengine,” alisema Hessein Machazi.
Alisema kikubwa kinachotakiwa ni sapoti kutoka
kwa mashabiki na kwamba wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi ambavyo
amewaandalia.
Mbali na kibao hicho, Hussen Machozi kwa sasa
anatamba n akibao chake cha ‘Addicted’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo
mbalimbali vya redio na runinga.
No comments:
Post a Comment