KAZI ya ukaguzi wa mita za umeme kwa wateja wa Shirika La
umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Shirika hilo Temeke iliendelea tena jana na kuwakatia
umeme watu watano
baada ya kukuta na makosa mbalimbali.
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya operesheni
ya ukaguzi wa mita hizo uliofanyika jana Mtoni Kwa Azizi Ally eneo la
Relini
msimamizi wa zoezi hilo Johari Nasibu, alisema jumla ya nyumba 80
walizifanyia
ukaguzi.
“Kama
tunavyofanya siku zote kwenye zoezi hili leo hii
tumefanya hapa mtoni eneo la relini tumefanikiwa kukuta mita nane zikiwa
na
makosa mbalimbali na hatua za haraka tulizo zichukua ni kuwasitishia
huduma
kwanza kabla ya kufanya tathmini ya hasara tuliyopata ili waweze
kutulipa na
kama hawajalipa tunawafikisha mahakamani” alisema Nasibu.
Akifafanua zaidi makosa waliyowakutanayo wateja hao
aliyataja kuwa ni pamoja na Wizi kwa njia ya kuharibu mita wateja
watano, Kuiba
umeme kabla haujafika kwenye mteja mmoja na Kujiunganishia umeme bila ya
kufuata taratibu wateja wawili.
Aidha Johari alisema kiasi kikubwa cha umeme kimeibwa na
shirika lazima litawachukulia hatua kali za kisheria endapo hawatakubali
kulipia umeme walioutumia kwa kipindi chote.
No comments:
Post a Comment