Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 24, 2011

MATAKA AJIVUA GAMBA ATCL

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATC), David Mataka (60) ametangaza kustaafu.
Mataka alitangaza hatua yake hiyo katika ukumbi wa mikutano wa ATC mbele ya waandishi wa habari huku akimtupia lawama Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa kwa kumsimamisha kazi kipindi cha utawala wake.
Mataka alikumbwa na kadhia hiyo wakati wa utawala wa Mkapa alipokuwa mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) na kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi kutokana na kashfa ambazo zilikuwa na lengo la kumchafulia jina.
"Sijafukuzwa kazi ila nimestaafu kutokana na umri wangu kisheria kunitaka nifanye hivyo.....Nimezaliwa May 11 , 1951 , hivyo tayari nimetimiza miaka 60", Alisema.
http://mamapipiro.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...