Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 17, 2011

ZANTEL YAJA NA ZARI SMS


KAMPUNI ya simu za mkononi Zantel imezindua promosheni mpya ya 'ZARI SMS'ikiwa ni baada ya 'Hamisi Ma SMS' kugawa mamilioni ya fedha kwa washindi .

Promosheni hiyo kubwa iitwayo 'ZARI SMS' ilizinduliwa mwishoni mwa wiki na itakuwa na jumla ya zawadi zenye thamani ya sh.milioni 160 zitakazokuwa zikitolewa kwenye
droo za kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa muda wa siku 84 ambapo wateja 92 watajishindia zawadi tofauti katika promoshen hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bw. Brian Karokola akizungumza na waandishi wa habari mwisho mwa wiki alisema nia ya kuanzisha promosheni hiyo ni kuwashukuru wateja wao wa Zantel na kuwapa fursa kujishindia Zawadi tofauti.


“Promosheni ya ZARI SMS' tunaamini itabadili maisha ya wateja wetu kwa njia moja au nyingine, kupitia zawadi tulizowaandalia kama fedha taslim,simu aina ya Blackberry na laptop ambazo tayari zimeunganishwa
na intaneti kwa mwaka mzima,”alisema.


Alisema kushiriki katika promosheni hiyo mteja wa Zantel atatuma SMS yenye neno ZARI kwenda 15587 na atapata nafasi ya kujishindia sh.milioni 1 kila siku kwa mshindi mmoja kupitia droo,sh. milioni 2 kila wiki kwa mshindi mmoja aliyetuma SMS nyingi zaidi na sh. milioni

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...