Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 18, 2011

TBL YAKARABATI HOSPITALI YA MWANANYAMALA


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana akizungumza na maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), baada ya kupokea jengo la wodi ya kinamama katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam juzi lililokarabatiwa kwa msaada wa TBL. Kutoka kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Bi. Doris Malulu, Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Bi. Emma Oriyo, Muuguzi wa hospitali hiyo, Bi. Baraka Kapinga na Mhandisi John Malisa wa Kampuni hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana (mbele), akisindikizwa na Mhandisi wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. John Malisa (kulia) kukagua choo cha wodi ya kinamama ya Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam, kilichokarabatiwa na TBL.Kushoto ni Meneja Miradi Maalum wa TBL, Emma Oriyo. Hafla hiyo ya kukabidhi choo na jengo la akinamama ilifanyika juzi hospitalini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Jordan Rugimbana (kushoto), akimpa mkono wa pongezi Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi Doris Malulu, baada ya kupokea juzi jengo la wodi ya kinamama la Hospitali ya Mwananyamala lililofanyiwa ukarabati kwa msaada wa TBL. Wengine kulia ni Mhandisi wa TBL, Bw. John Malisa, Meneja Miradi Maalumu wa Kampuni hiyo, Bi.Emma Oriyo na Muuguzi wa Hospitali hiyo, Baraka Kapinga

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...