Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 18, 2011

UN HABITAT Yawapa Semina Vijana Wasanii Chipukizi

Mwakilishi wa Shirika la Makazi laUmoja wa Mataifa (UN HABITAT) Philimon Mutashibirwa akifungua semina siku moja kwa Vijana wasanii chipukizi kutoka wilaya za mkoa wa Dar es Salaam leo asubuhi katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaa. Semina hiyo imeandaliwa na kituo cha Vijana cha UN Habitat cha jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa elimu vijana chipukizi wanaojishughulisha na sanaa za aina mbali mbali kutambua wajibu na haki zao katika kazi zao za sanaa kwa lengo la kuziboresha ili ziwaletee tija. Katika ufunguzi huo mgeni Rasmi Philimon Mutashibirwa aliwaasa vijana kuwa makini, kutia nia sambamba na kujiwekea malengo ya muda mfupi, wa kati na malengo ya muda mrefu ili waweze kufanikisha malengo yao. Kushoto ni Afisa Vijana Wilaya ya Temeke Anna Malika. Wa kwa kwanza kulia ni Afisa kutoka BASATA Omar Mayanga na wa pili kushoto ni Gadi Karugendo Mratibu wa Vijana kutoka Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa kituo cha Dar es Salaam.

Mratibu wa Kituo cha Vijana cha jijini Dar es Salaam, Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN HABITAT) Gadi Karugendo akielezea jambo kw vijana wasanii chipukizi kutoka katika wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke leo asubuhi katika ukumbi wa Karimjee. Karugendo aliwataka vijana kuwa na uthubutu sambamba na kujiamini ili waweze kutimiza malengo yao. Pia aielezea kuwa sanaa ni ajira tosha na ikitumiwa vizuri hupelekea vijana wengi kuishi maisha bora na huwaepusha vijana kuingia katika makundi hatarashi katika jamii.Aliwahakikishia vijana hao kuwa yeye kama mratibu wa wa Vijana wa UN Habitat atahakikisha kuwa vijana wanaelekezwa na kupatiwa fursa zote wanazostahili ili waweze kuboresha maisha yao.

Mzee Omar Mayanga, Afisa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akiwa ndiye mwezeshaji mkuu wa Semina hiyo akitoa mada kwa vijana kuhusu umuhimu wa msanii katika nyanja mbali mbali za maisha. Mzee Mayanga aliwaeleza Vijana wasanii chipukizi kuwa licha ya sanaa kuwa ni ajira bali pia ni wasanii na kazi zao za sanaa ni kioo cha jamii kwani hubaki kuwa mfano wa kuigwa na jamii nzima Akiongeza kusema alisema kuwa kazi za sanaa ni mwongozo tosha kwa maisha ya vijana, hivyo aliwaasa vijana hao kutia nia katika kazi zao za kisanii na kutokata tamaa katika kupambambana na changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo ili wapige hatua za maendeleo.

Mlemavu wa ngozi (albino) akitoa burudanii kwa Mgeni rasmi na vijana wasanii chipukizi waliohudhuria semina hiyo ya siku moja. Mlemavu huyu wa ngozi ni mahiri kwa kuigiza sauti za makabila mbali mbali hapa nchini.

Baadhi ya vijana wasanii chipukizi wakiwa katika semina hiyo leo asubuhi katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha:Victor Makinda)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...