Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 8, 2011

VODACOM FOUNDATION YATOA MSAADA WA MADAWATI 50 KWA SHULE YA MSINGI UNUNIO


Ofisa Elimu wa kata ya kunduchi, Geradine Ishengoma ,akiwasisitiza jambo baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio kutunza madawati 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 4 baada ya kukabidhiwa ba msaada na Vodacom Foundation na Ofisa wa mfuko huo Grace Lyon (kulia).

Ofisa wa mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom, (Vodacom Foundation) Grace Lyon, akifurahi na baadhi ya mwanafunzi wa darasa la kwanza Jamila Hamis wa shule ya msingi ununio iliyopo kata ya kunduchi wilaya Kinondoni jijini Dares Salaam baada ya kukabidhi madawadi 50 yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 4,wengine ni baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio iliyopo Kata ya Kunduchi wilaya ya Kinondoni jijini Dares Salaam wakifurahia msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Vodacom Foundation yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 na kukabidhiwa na Afisa wa mfuko huo, Grace Lyon hayupo pichani.Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ununio iliyopo kata ya kunduchi Wilaya ya Kinondoni wakisikiliza jambo kwa umakini kutoka kwa Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 yenye ya zaidi ya Shilingi million 4.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...