Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, May 18, 2011

MHE. NCHIMBI ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA MUZIKI AINA ZOTE….!!!

Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi (MB) akizungumza leo na wasanii wote wa sanaa za muziki wa aina zote wakiwemo wa kizazi kipya, bendi, disko, asili, taaribu n.k. kuhusiana na mikakati ya kukuza na kuinua sanaa hiyo. Katikati ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utamaduni Angela Ngowi. Hapo kesho Mhe.Waziri anatarajia kukutana na kuzungumza na wasanii wa sanaa za filamu, maonyesho, na ufundi.

Lengo kuu la mikutano hii kati wa Mhe. Waziri na wasanii ni kuongelea maendeleo ya fani ya sanaa hapa nchini.

Pichani Juu na Chini Baadhi wa wasanii wa muziki wa aina zote waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

‘Penye wengi pana mengi’ Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Bob Junior akisikiliza nasaha za Mhe. Waziri kwa staili ya aina yake kupitia simu ya kiganjani.


Msanii kizazi kipya Kassim akitoka nje ya ukumbi mara tu baada ya kumalizika mkutano huo.

Baadhi ya wasanii kizazi kipya wakiuza nyago nje ya ofisi za BASATA.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...